January 08, 2015


Mercedes-F125-Hydrogen-Concept
Moja ya vilio vikubwa sehemu za kazi ni pale ambapo inatokea teknolojia halafu inachukua nafasi ya kazi za watu kama utani!
Zilipokuja computer ilikuwa zengwe, wapo ambao walijikuta hawana ajira sasa hii kutoka Ujerumani imenishtua kidogo.
Kampuni ya kutengeneza magari Ujerumani ya Daimler imejipanga kutengeneza gari ya kisasa ambayo itakuwa na uwezo wa kujiendesha yenyewe huku ikiwa na uwezo wa kuchukua abiria wanne.

Mercedes-F125-Hydrogen-Concept  
Gari hii ambayo imeundwa kwa muundo wa kisasa itakuwa ya kipekee huku ikiwa na usukani kama magari mengine tofauti na lile gari la google ambalo halina usukani, hili lina siti ya dereva na siti za abiria, siti zote zina uwezo wa kugeukiana na kufanya watu waliokaa ndani ya gari kutazamana kama wako kwenye meza moja.

APTOPIX Gadget Show Mercedes Benz 

Mercedes-F125-Hydrogen-Concept

video hii hapa cheki mwenyewe itakavyokuwa.
                

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE