March 28, 2015


Marubani wawili wa Saudi Arabia waliokolewa na wanajeshi wa Marekani baada ya helikopta yao kupata ajali katika Bahari ya Sham

NKwa mujibu wa taarifa iliotolewa na vyombo vya habari ni kwamba, marubani wawili wa Saudi Arabiawaliokolewa na wanajeshi wa Marekani baada ya helikopta yao kupata ajali kutokana na matatizo ya kiufundi na kuanguka katika bahari Sham Ijuma. 

Shirika la habari la serekali lilifahamisha kuwa marubani hau walitumia mbinu mbadala baada ya kuona matatizo ya kiufundi na kufyatua vite vya uokozi baada ya kuona itilafu katika ndege ya kivita F-15Swaliokuwa wakitumia.

Taarifa rasmi zinafahamisha kuwa marubani hao wapo katika hali nzuri na salama baada ya kuokolewa na wanajeshi wa Marekani.

Wizara ya ulinzi ya Marekani ilifahamisha kuwa marubani hao waliokolewa na jeshi la Marekani katika enea la kimataifa na helikopta ya kimarekani baada ya ajali kutoka Djibouti.

Mfalme wa Saudi Arabia alitoashukrani kwa rais wa Marekani kwa kuwaokoa marubani hao.

Saudi Arabia inashirikiana na nchi za Ghuba kupambana na wapiganaji wa Houthis

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE