March 01, 2015

 
  Kuelekea uchaguzi mkuu 2015 nchini Tanzania, watu mbalimbali wanasia na wasanii wameanza kutangaza nia zao za kutaka nyazifa mbalimbali katika maeneo yao. Mbarala Abdallah Maharagande ni miungoni mwa wanasiasa wakongwe mkoani Morogoro na kipenzi cha watu wengi sana jimbo la Morogoro mjini kutokana na utashi wake wa kisiasa, kujumuika na lika mbalimbali za watu na   kujitolea kwake katika jamii hasa alipokuwa Diwani wa Kata ya Sultani Area na hatimaye kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Morogoro mjini kupitia chama cha wananchi CUF 2005 na kuleta upinzani mkubwa sana wa kisiasa dhidi ya CCM
  
 Baada ya kushindwa Maharagande alionekana na CUF Taifa na kuamua kumchukua na kufanya kazi za kitaifa kutokana na kujituma kwake. Safari hii baada ya ushawishi wa wakazi wa Morogro, Maharagande ameatngaza rasmi kurudi na kuwania nafasi ya Ubunge katika jimbo la Morogoro mjini jimbo ambalo kwa sasa wengi huliita jimbo la Maharagande. Katika dhamira yake ya dhati juu ya jimbo hilo, Mbarala ametaja vipaumbele vyake vya awali vilivyomshawishi na kuamua kugombea Jimbo hilo ambalo limekaa chini ya CCM kwa muda mrefu sasa.

1. KUSHINDA JIMBO
2. KUTENGENEZA KURA ZA RAIS WA UKAWA ZAKUTOSHA.
3. KUUNDA HALMASHAURI KWA KUPATA MADIWANI WA KUTOSHA WA UKAWA.
4. KUENDELEZA UJENZI WA DEMOKRASIA NA KUIMARISHA UKAWA.
5. MUENDELEZO WA DHANA YA UKOMBOZI- TULICHOKIAMINI MIAKA 20 ILIYOPITA HATUJAYUMBA NACHO.
6. KUWATUMIKIA WANANCHI WA JIMBO KWA UMAKINI NA WELEDI WA HALI YA JUU NA KUWEKA MISINGI THABITI YA MAGEUZI NA MABADILIKO YA KISIASA NA KIUCHUMI.
7. KUSIMAMIA UTENDAJI WENYE KULETA MAENDELEO NA KUTOA ATHARI NZURI KWA WANANCHI.(EFFECTIVE AND POSITIVE CHANGE

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE