
Chama cha rais mteule wa Nigeria
APC, kimesajili ushindi mkubwa wa majimbo 19 kati ya 29 katika matokeo
ya hivi punde yaliyotangazwa na tume huru ya uchaguzi INEC.
Awali
INEC ilikuwa imethibitisha kuwa chama cha rais mteule The All
Progressives Congress (APC) kilikuwa kimetwaa miji mikuu ya Lagos Kaduna
na na Katsina.
Ushindi huo ni dhidirisho ya kuwa chama kinachoondoka madarakani cha Rais Goodluck Jonathan PDP kimepata kichapo chake kikubwa zaidi tangu kukamilika kwa utawala wa kijeshi mwaka wa 1999.
Jenerali mstaafu Muhammadu Buhari anatarajiwa kuapishwa rasmi kama rais wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika mwishoni mwa mwezi Mei.
Mwandishi wa BBC aliyeko Abuja Bashir Saad Abdullahi anasema kuwa chama cha jenerali mstaafu Muhammadu Buhari The All Progressives Congress (APC)
Kilihifadhi jimbo la Lagos mbali na kutwaa majimbo zaidi ya Kaduna naKatsina.
Ushindi huu wa majimbo zaidi unaiongezea pondo serikali mpya haswa baada ya kutwaa ushindi mkubwa dhidi ya Rais Goodluck Jonathan.
Matokeo kamili ya kura za majimbo 39 na magavana 29 unatarajiwa kutolewa baadaye.
Lagos
Uchaguzi huu wa majimbo umeendeleza dhana ya kuwa APC itazoa maeneo wakilishi mengi kufuatia ushindi wa wa kihistoria wa jenerali mstaafu Muhammadu Buhari.
Siku ya jumapili, tume huru ya uchaguzi nchini humo (Inec) ilitangaza rasmi kuwa chama cha Jenerali mtaafu Buhari APC ilikuwa imetwaa jimbo la Lagos mbali na kushinda ugavana wa majimbo ya Kaduna na Katsina majimbo
ambayo yaliongozwa na kudhaniwa kuwa ni ngome ya PDP
Vilevile hii ndio itakayokuwa mara ya kwanza kwa chama ambacho sio PDP kuwahi kuiongoza majimbo ya Kaskazini mwa taifa hilo.
Uongozi wa majimbo 36 unaumuhimu mkubwa haswa kiuchumi kwani magavana wengi katika maeneo yenye utajiri mkubwa wa mafuta huwa wana makadirio ya bajeti makubwa hata zaidi ya mataifa mengine ya Magharibi mwa Afrika.
Chama cha PDP hata hivyo kilihifadhi jimbo la Rivers
0 MAONI YAKO:
Post a Comment