Pichani
juu na chini ni Mh. January Makamba akihutubia wanachi na wanachama wa
CCM mkoani Ruvuma mara baada ya kabidhiwa fomu yenye sahihi za wanachama
waliomdhamini.
Na Mwandishi Wetu
MBUNGE
wa Bumbuli, January Makamba amewataka makada wote waliomba ridhaa ya
kuteuliwa kugombea nafasi ya urais ndani ya Chama kuwa wanakiacha chama
hicho kuwa salama baada ya mchakato huo kukamilika.
January,
aliyasema hayo baada ya kupokea orodha ya wanachama wa chama hicho,
katiaka Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa Ruvuma jana, ambapo wanachama
3500 walijitokeza kumdhamini.
Alisema
hivyo kwa vile kuna wapo waomba ridhaa ambao wanadai kuwa endapo
hawatateuliwa katika nafasi hiyo kuna hatari chama kikasambaratika.
Alisema,
chama hicho kinahitaji kupata mgombea ambaye atahakikisha kuwa nama
hicho kinabaki salama na kwambapia atawaongoza watanzania wote bila
kujali dini wala kabila zao, akibainisha kuwa yeye ndio sahihi katika
kudumisha hayo.
”Mimi
siamini siasa za kupakana matope kwani wote ni wanachama wa chama
kimoja na mwisho wa siku tutapata mgombea mmoja na tutahitajika kumpigia
kampeni”alisema Jamuary.
January,
alisema kama wagombea watapakana matope katika mchakato huo wa kuomba
ridhaa kwa wanachama, anaamini wakati ukifika wa kumfanyia mteule
utakuwa mgumu kwani itakuwa siyo rahisi kumfanyia kampeni ambaye tayari
umekwisha kumpaka matope.
“Niwaombe
muwapime wagombea ambao wameonekana wakiomba nafasi hiyo kwa mbwembwe
kwani hatawatakapopata nafasi hiyo wataongoza kwa mbwe jambo ambalo
wananchi hawalihitaji”alisema Jamnuary.
January,
alisema kuwa chama hicho kiko makini na hakitamteua mgombea kwa woga
kama inavyodaiwa na baadhi ya wagombea kwamba wasipochaguliwa chama
hicho kitasambaratika jambo ambalo siyo sahihi.
Alisema kuwa anaamini kuwa chama hicho kitamteuwa mgombea ambaye ni muadilifu, atakuwa rahisi katika kumnadi kwa wananchi.
Akizungumzia,
mkoa wa Ruvuma, January, alisema mkoa huo hivi sasa unakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo tatizo la umeme na upande wa hospitali ya
Mkoa.
Alisema
kwa vile matatizo hayo anayatambua, pindi atakapopewa ridhaa na chama
na kuchaguliwa kuwa rais atahakikisha mkoa huo unaingizwa katika gridi
ya Taifa kama ilivyo kwa mikoa mingine.
Katika hatua yingine, juzi mkoani Njombe, January alipata wadhamini 84.
January,
alisema anaamini atakapokuwa rais atakuwa na uwezo wa kuamua mambo
makubwa yanayolihusu taifa ukilinganisha na nafasi aliyosasa kwani
inamopaka katika maamuzi ya kushughulikia mambo mbalimbali ya Taifa.
Mh January Makamba
akihutubia wanachi na wanachama wa CCM mkoani Ruvuma ndani ya ukumbi wa
ofiswi kuu ya chama hicho mkoani Ruvuma. kuanzia kushoto ni mke January
Makamba, Ramona Makamba, katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho
na kulia ni mwenyekiti wa CCM mkoa, Odo.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho akimkabidhi fomu yenye majina na
sahihi za wanachama waliomdhamini Mh. January Makamba. Makabidhiano hayo
yamefanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi kuu ya CCM mkoa wa
Ruvuma.
Mh
January Makamba na mkewe, Ramona Makamba wakipeana mikono na wanachama
wa CCM mkoa wa Ruvuma waliofika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi
kuu ya CCM mkoa wa Ruvuma.
Katibu wa CCM mkoa wa Ruvuma, Verena Shumbusho akiwakaribisha mkoani Ruvuma Mh January Makamba na mkewe, Ramona Makamba. |
0 MAONI YAKO:
Post a Comment