June 17, 2015

Wema
Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Bi Wema Sepetu akipokea maelekezo kutoka kwa katibu wa CCM wilaya ya Ikungi,Bwana Alluu Ismaili Segamba kabla ya kuongea na wananhi pamoja na wanachama waliohudhuria kwenye mkutano huo. (Picha zote na Jumbe Ismailly).

Na Jumbe Ismailly,Ikungi     
Hatimaye aliyewahi kuwa, Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Wema Spetu ameanza safari maalum ya kuwania nafasi ya Ubunge kupitia chama cha Mapinduzi Mkoani Singida, ambapo ni chimbuko la Mama yake Mzazi.
Wema yupo aliwasili Mkoani Singida huku akifanya harakati mbalimbali za kichama ikiwemo uhamasishaji wa  Wananchi kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
Aidha, wakati wa safari hiyo ya Wem alipata wasaha wa kuhudhuria mkutano mkubwa wa hadhara, uliofanyoka katika viwanja vya Ghafla.  Katika mkutano huo,  kwa upande wake Katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Aluu Ismaili Segamba alisikitishwa na hali ya shule ya sekondari ya kata ya Ikungi,wilaya ya Ikungi,Mkoani Singida kutokana na kuwa hatarini kufungwa wakati wowote kutokana na kukosa choo cha wanafunzi pamoja na walimu wa shule hiyo kwa muda mrefu sasa.
Segamba alitoa kauli hiyo kwenye mkutano  huo na kufafanua kuwa hali ya shule ya sekondari Ikungi hivi sasa ni mbaya sana kutokana na wanafunzi pamoja na walimu wao kutokuwa na sehemu za kujisaidia kufuatia viongozi na wazazi wa shule hiyo kushindwa kujenga matundu ya vyoo kwa ajili ya matumizi ya shule hiyo.
“Akazungumza Sigamba na magamba sijui na kitu gani tumeenda shule,kwanza nikiri ni kweli nimeenda kwenye shule ya sekondari ya Ikungi nimekula chakula na wanafunzi na walimu,lakini hali ya shule ya sekondari ya Ikungi ni mbaya shule itafungwa kwa kukosa vyoo”alisema kwa kujiamini Segemba.
“Kama wazazi mpo hapa,kweli siyo kweli…kweliii,shule itafungwa pale kwa kukosa vyoo halafu mna mbunge anakataza michango,sasa pale naenda kujisaidia mimi au watoto wenu?”alihoji katibu huyo huku akionyesha kukerwa na hali hiyo.
Alisema shule kukosa vyoo ni suala la aibu wanafunzi pale wa kidato cha nne na tano hawana pakujisaidia,halafu anakuja kulalamika kuwa katibu wa CCM ameenda pale shuleni kutafuta kura,jambo ambalo hakuwa tayari kukubalinanaalo.
Naye Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Ikungi (MNEC),Jonathani Njau aliwakumbusha wakazi wa kata ya Ikungi juu ya umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapigakura,ili wakati ukifika wajitokeza pia kupiga kura.
“Lakini tunatakiwa tukajiandikishe kwa wale ambao tuna sifa
ya kupiga kura,kwani watu wengi wanadhani zoezi la kujiandikisha ni la kisiasa siasa tu,la mzahamzaha si kweli.”alisisitiza mjumbe huyo.
Hata hivyo Njau pamoja na kutokuwepo kwa mikakati yeyote madhubuti ya kulirudisha jimbo hilo kutoka CHADEMA,lakini alijikuta akitamba kuwa mwaka huu CCM bado kitashinda na hapo Ikungi ndiyo watashinda zaidi.
“Kama mlidanganywa zile sarakasi za 2010 mwaka huu hakuna,hazitakuwepo na rafiki zangu,nawabip vijana wa Ikungi kuwa uhuni mlioufanya mwaka 2010,mwaka huu mlie tu,CCM ya mwaka huu imejitosheleza”alisisitiza Njau.
wer
Msanii wa Bongo Movie na Miss Tanzania 2006,Bi Wema Sepetu katika mapokezi yake alipofika kwenye viwanja vya ghala ulipofanyika mkutano wa hadhara.
wev
Miss Tanzania 2006 na Msanii wa Bongo Movie,Wema Spetu(wa pili kutoka kushoto) akishiriki kuimba wimba wa kimila mara baada ya kukaribishwa kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi kujiandikisha

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE