February 25, 2016

                            

Meli moja ya shehena aina ya MV BOURBONiliyokuwa na baharia wa Urusi imeripotiwa kutekwa nyara na maharamia wa Nigeria karibu na pwani ya kisiwa cha Bonny.

Raia huyo wa Urusi ambaye bado hajatambulika, anasemekana kuchukuliwamateka pamoja na baharia mwenzake ambaye ni raia wa Nigeria.

Meli hiyo iliyotekwa nyara siku ya Jumatano, iliweza kuokolewa na kikosi cha wanamaji chaNigeria baada ya kupatikana maili 55 kutoka pwani ya Niger Delta.

Mabaharia hao wawili wanahofiwa kuchukuliwa mateka na maharamiwa baada ya kukosekana ndani ya meli hiyo.

Operesheni ya kuwatafuta mabaharia hao inaarifiwa kuanzishwa katika pwani hiyo

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE