Wanajeshi wa Israel wameripotiwa kumuua afisa wao mmoja wa jeshi kimakosa wakati wa mapambano na Wapalestina.
Kulingana na taarifa zilizotolewa na kituo cha redio ya Israel, iliarifiwa kuuawa kwa afisa huyo mkuu wa jeshi kwa kufyatuliwa risasi na wanajeshi wenzie walipokuwa wakiwalenga Wapalestina.
Jeshi la Israel pia lililotoa maelezo na kuthibitisha kuuawa kwa afisa huyo mkuu kwenye mapambano na Wapalestina.
Wapalestina waliojeruhiwa kwenye tukio hilo nao wanaarifiwa kufikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment