Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), imeendelea leo kwa michezo kadhaa huku mchezo ulikuwa ukitazamwa na mashabiki wengi wa soka ni kati ya Azam iliyokuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo ulicheza katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaa.
Mchezo huo umemalizika kwa sare ya goli mbili kwa mbili.
Azam ndiyo ilikuwa ya kwanza kuona lango la Yanga dakika ya 12 baada ya beki wa Yanga, Juma Abdul kujifunga dakika ya 12 na dakika ya 28 beki huyo akaisawazishia Yanga baada ya kupiga shuti kali lililomzidi nguvu goli kipa wa Azam, Aishi Manula.
Yanga ilifanikiwa kupata goli la pili kupitia kwa Donald Ngoma katika dakika ya 41 baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi kutoka kwa Amissi Tambwe goli lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili dakika ya 70, John Bocco aliiandikia Azam goli la 2 na hadi mchezo huo unamalizika, Azam 2 na Yanga 2.