Baadhi ya wananchi wasio na uwezo wakiwemo wazee katika kitongoji cha SOWETO katika kijiji cha Kilosa wilayani Nyasa Mkoani Ruvuma wamelalamikia kubaguliwa kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini wa TASAF wilayani humo.
Wameyazungumza hayo wakati wakizunguza na ITV katika kijiji cha
Kilosa wilayani Nyasa na kusema pamoja na kwamba wao ni maskini lakini
TASAF wamekuwa wakiisikia kwenye vyombo vya habari bila kuwafikia.
ITV pia imezungumza na Bibi mmoja anayesumbuliwa na magonjwa ya
moyo na mapafu kuwa na vidonda ambapo analalamikia kukosa ruzuku ya
TASAF.
Akijibu malalamiko hayo mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
wilaya ya Nyasa Bw.Jabir Shekimweri anasema Halmashauri yake imepangiwa
kutoa ruzuku ya TASAF kwa vijiji hamsini kulingana na vigezo
vilivyowekwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment