Wiki
kadhaa zilizopita kuliripotiwa taarifa kuwa Mtanzania amepigwa risasi
nchini Marekani na kupoteza maisha, aidha kumeripotiwa taarifa nyingine
kuwa Mtanzania, Andrew Sanga amepigwa risasi Houston, Texas, Marekani.
Katika
taarifa ambayo imetolewa na Msemaji wa HTC, Cassius Pambamaji imeeleza
kuwa Sanga alipigwa risasi na watu wasiofahamika na kwa sasa Polisi wa
nchini Marekani wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo ili waweze
kuwafahamu waliohusika katika tukio hilo.
Kwa
upande wa msemaji wa familia, Prosper Kiswaga amesema kwa sasa Sanga
yupo Hospitali ya Memorial Hermann Southwest, Houston, Texas katika
Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na hali yake bado sio nzuri.
Ameeleza
kuwa kwa sasa anayeruhusiwa kumwona Sanga ni mke wake, Emmy Matatu na
hivyo kuwaomba Watanzania kuungana na wanafamilia kwa ajili ya kumuombea
ndugu Andrew Sanga ili aweze kurejea katika hali yake ya awali.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment