Mbunge
wa jimbo la Chalinze mkoa wa Pwani Ridhiwani Kikwete alipokwenda jana
kutembelea shule ya sekondari Chalinze baada ya bweni la wanafunzi wa
kiume kuungua kutokana na shoti ya umeme. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Bweni lililoongua kwa shoti ya umeme jana
WANAFUNZI
65 wa shule ya sekondari chalinz e iliyopo Wilayani Bagamoyo mkoani
Pwani wamenusurika kifo baada ya bweni lao kuteketea kwa moto wakati
wao wakiwa darasani kwa ajili ya kujisomea masomo ya usiku.
Akizungumza
na MWANDISHI WA HABARI HIZI kwa njia ya simu mkuu wa wilaya ya Bagamoyo
Majid Mwanga alisema tukio hilo limetokea april 17 majira ya saa 3:20
usiku .
Mkuu
huyo alisema chanzo cha moto huo inadaiwa ni shoti ya umeme ambayo
imesababisha moto huo kuteketeza vifaa vyote vikiwemo
magodoro,vitanda,vitabu katika bweni hilo.
Mwanga
akizungumzia kuhusiana na juhudi za serikali ambazo tayari
wameshazichukua hadi sasa alisema wanawahifadhi wanafunzi hao katika
jengo lingine la muda ambalo lilikuwa linatumika kwa chakula.
Alisema
kuwa pia serikali ya mkoa imeshaanza kuwasiliana na wadau mbalimbali
ambao watasaidia kununua vifaa vya ujenzi kwa kusaidiana na serikali ili
kujenga bweni jingine.
“Siwezi
kusema hali ni nzuri kutokana na watoto wameunguliwa vifaa vyao,ni
hasara katika jengo pia kwahyo kilichopo sasa ni kumshukuru mungu kwa
wanafunzi hawa kunusurika”alisema Mwanga.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo Chalinze Hussein Mramba alikiri kutokea kwa tukio hilo
Alisema mkandarasi wa halmashauri ya wilaya hiyo bado anaendelea na tathmini ya miundombinu iliyoungua.
Shule
ya sekondari Chalinze ina jumla ya idadi ya wanafunzi 1,151 kati yao
65 kwa sasa wameunguliwa na vitu vyao vyote hivyo kunahitajika juhudi za
jamii,wadau na serikali katika kuhakikisha wanatoa msaada wa hali na
mali .
0 MAONI YAKO:
Post a Comment