Mkongwe wa Liverpool ambaye kwa sasa anakipiga LA Galaxy ya Marekani, Steven Gerrard ameweka wazi kuwa atarejea timu yake ya zamani Liverpool mapema zaidi baada ya kudumu kwa misimu miwili katika ligi Marekani.
Akiwa katika kipindi cha maswali na majibu kutoka kwa mashabiki, Gerrard amesema kuwa anafurahia maisha ya LA Galaxy lakini anaamini ipo siku ataichezea Liverpool kwa mara nyingine.
“Nitakwenda nyumbani, sitaki kuwa katika tetesi ambazo siyo sahihi, nina furaha na sehemu niliyopo sasa lakini upo wakati nitaiwakilisha klabu ya Liverpool,” alisea Gerrard.