Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Jamii nchini ‘Tanzania
Bloggers Network’ – TBN inawaomba wanachama wake wote kutotumia taarifa
ama habari au picha yoyote kutoka katika mkutano wa maadhimisho ya Uhuru
wa Vyombo vya Habari (WPFD) unaofanyika kitaifa mkoani Mwanza.
Kamati Kuu ya Uongozi TBN imefikia hatua hiyo jana baada ya
kujadiliana na kujiridhisha kuwa kumekuwepo na taasisi za tasnia ya
habari ambazo zimekuwa zikiwatenga wanahabari wa mitandao ya kijamii
(bloggers) na kutotambua umuhimu wao wakati sehemu kubwa ya taarifa
mbalimbali nchini husambazwa na mitandao hiyo.
TBN iliyosajiliwa rasmi serikalini Aprili 2015 na kupewa namba ya
usajili; S. A 20008 inawataka wanachama wake kutotoa ushirikiano wa sina
yoyote kwa taasisi ambazo zinawatenga bloggers.
Tunasikitika kufikia hatua hii ila hamna jinsi. TBN itasikitika na
kumshangaa mwanachama wake au blogger asiye mwanachama kutounga mkono
agizo hili, na kwenda kinyume na agizo hili. Muda umefika ‘Bloggers’
kudai heshima, kutambulika na kuthaminika kama tasnia ya habari ingine
yoyote.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment