May 01, 2016

Simba 33 waokolewa Peru na kusafirishwa Afrika Kusini
Jumla ya simba 33 waokolewa kutokana na unyanyasaji Peru na kusafirishwa kwa ndege hadi Afrika Kusini.
Wanyama hao walikuwa wanatumiwa nchini Peru kufanya mchezo wa sarakasi.
Hata hivyo serikali ya Peru imepiga marufuku utumiaji wa wanyama katika mchezo huo wa sarakasi jambo ambalo lilishinikiza kusafirishwa kwa simba hao Afrika Kusini.
Usafirishaji wa wanyama hao ulifanywa na shirika la kutetea maslahi na haki za wanyama (ADI) chini ya uongozi wa mkurugenzi mkuu Jan Creamer.
Kwa mujibu wa Jan wanyama hao waliotumiwa katika mchezo huo daima walikuwa wagonjwa na pia majeraha ya mara kwa mara.
Licha ya hayo wanyama hao walikuwa hawapewi chakula cha kutosha na kwa sababu hiyo walikuwa na matatizo ya utapiamlo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE