May 28, 2016

Madrid-UCL 6
REAL Madrid wametwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa penalti 5-3 baada ya sare ya 1-1 dhidi ya mahasimu wao, Atletico Madrid usiku wa kuamkia leo Uwanja wa San Siro, Milan, Itali.
Kipa Keilor Navas Gamboa alijitanua vizuri langoni na Juan Francisco Torres Belen ‘Juanfarn’ akaona lango dogo na kugongesha nguzo ya pembeni penalti ya nne ya Atletico.
Cristiano Ronaldo akaenda kwa kujiamini kupiga penalti ya mwisho ya Real Madrid na kumtungua kipa Jan Oblak wa Atletico kuwapa Magalactiico taji la 11 la Ligi ya Mabingwa.
Wengine waliofungaa penalti za Real Madrid ni Lucas Vazquez, Marcelo, Gareth Bale na Sergio Ramos, wakati Atletico zimefungwa na  Antonio. Griezmann, Gabi na Saul.



 Sergio Ramos lifts the Champions League trophy after Real Madrid came out on top against Atletico Madrid 
Nahodha wa Reald Madrid, Sergio Ramos akiinua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuifunga Atletico Madrid kwa penalti 5-3 usiku huu Uwanja wa San Siro

Mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa England, Mark Clattenburg aliyesaidiwa na Simon Beck na Jake Collin, Real Madrid walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa beki wake na Nahodha, Sergio Ramos dakika ya 15 aliyemalizia mpira wa kichwa wa winga Gareth Bale. Baada ya bao hilo, Real waliuteka mchezo na kupeleka mashambulizi mengi langoni mwa Atletico, lakini bahati haikuwa yao. Kipindi cha pili, kocha Diego Simeone wa Atletico alianza na mabadiliko, akimpumzisha kiungo Muargentina mwenzake Augusto Matias Fernandez na kumuingiza kiungo Mbelgiji Yannick Ferreira Carrasco. Mabadiliko hayo yalikuwa msaada kwa kikosi cha Simeone, kwani ni Carrasco aliyekwenda kuisawazishia Atletico dakika ya 79, akimalizia pasi ya Juan Francisco Torres Belen, maarufu kama Juanfran. Bao hilo ‘likauamsha’ upya mchezo huo, timu zote zikicheza ka nguvu na kasi kusaka bao la ushindi, lakini dakika 90 zikamalizika kwa sare ya 1-1. Awali ya hapo, mshambuliaji hatari wa Atletico Madrid, Antonio Griezmann alipaisha mkwaju wa penalti dakika ya 48 baada ya Fernando Torres kuangushwa na Pepe kwenye boksi. Kocha Mfaransa, Zinadine Zidane aliwapumzisha Karim Benzema, Daniel Carvajal na Toni Kroos kipindi cha pili na kuwaingiza Isco, Danilo na Lucas Vazquez. Katika dakika 30 za nyongeza timu zote zilicheza kwa tahadhari mno na mwishoni mwa mchezo, Simeone akawatoa Filipe Luis na Koke na kuwaingiza Lucas Hernandez na Thomas Teye Partey. Na baada ya kushinda kwa penalti 5-3, Real inafikisha mataji 11 ya Ligi ya Mabingwa, mengine ikitwaa misimu ya 1955–1956, 1956–1957, 1957–1958, 1958–1959, 1959–1960, 1965–1966, 1997–1998, 1999–2000, 2001–2002 na 2013–2014. Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; K. Navas, Sergio Ramos, Pepe, Marcelo, Daniel Carvajal/Danilo dk52, L. Modric, G. Bale, T. Kroos/ Isco dk72, Casemiro, Cristiano Ronaldo na K. Benzema/Lucas Vazquez dk77. Atletico Madrid; J. Oblak, Juanfran, Filipe Luis/ L. Hernandez dk109, D. Godín, S. Savic, Gabi, A. Fernández/Y. Carrasco dk46, Saul, Koke/T. Partey dk116, Fernando Torres na A. Griezmann.

Tazama picha zaidi hapa cjhini
Cristiano Ronaldo was  inevitably match winner as he kept his composure to strike home the crucial fifth penalty for Real

Ronaldo celebrates his winning spot kick after a tense penalty shootout resulted an 11th European Cup for Real Madrid

Ronaldo reserved himself for the fifth penalty and after Juanfran had struck the foot of the post he made no mistake 



Keylor Navas dives to his right and nearly gets fingertips onto Juanfran's penalty but it mattered not as the shot cannoned off the post

Juanfran trudges back to the centre circle after missing the crucial penalty to give Ronaldo the chance to clinch the victory for Madrid

Real Madrid players celebrate and their joy will spill long into the night after the club clinched their 11th European Cup at the San Siro

Atletico Madrid substitute Yannick Carrasco fires in from close range to bring his side level after 79 minutes of an absorbing encounter

The Belgian wheels away in delight having brought the scores level and the 22-year-old celebrated with his girlfriend on the sidelines 

Real Madrid defender Sergio Ramos celebrates giving his side the lead with a close range finish after 15 minutes at the San Siro

Ramos steers the ball underneath fallen keeper Oblak as Atletico failed to play to their strengths in the first 15 minutes of the encounter

The 30-year-old defender showed once more his appetite for the big occasion by scoring a crucial goal in the Champions League final
Madrid-UCL 5
Real Madrid imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuwanyoa watani zao Atletico Madrid kwa njia ya matuta. Hatua hiyo ya matuta ilikuja baada ya timu hizo kutoka sare ya 1-1 katika dakika 120 za mchezo. Katika mikwaju ya penalti Real Madrid ikaibuka na ushindi wa 5-4. Real Madrid ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 5 kupitia kwa Sergio Ramos bao lililodumu hadi dakika ya 79 pale Yannick Ferreira-Carrasco alipoisawazishia Atletico.

Soma zaidi hapa >>: http://www.saluti5.com/2016/05/matuta-yaipa-real-madrid-ubingwa.html
Copyright © saluti5

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE