June 25, 2016

2
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) amerejea nchi baada ya kumaliza ziara yake nje ya nchi na kukosoa ripoti ya uchaguzi mkuu uliyowasilishwa juzi kwa Rais Magufuli na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Maalim Seif ambaye alikuwa ziarani Marekani, Canada na kutembelea ofisi za Umoja wa Mataifa amesema kuwa ripoti iliyowasilishwa kwa Rais si mwarubaini wa mgogoro wa Zanzibar.
Maalim Seif aliyasema hayo mara baada ya kuwasili nchini na kueleza kuwa wale walioharibu uchaguzi huo ndio hao hao walioandaa ripoti hiyo kitu ambacho kamwe hakiwezi kuelezea ukweli wa mambo ulivyokuwa wakati wa uchaguzi.
Aidha kwa upande mwingine Maalim Seif amesema kuwa suluhisho pekee la mgogoro wa Zanzibar ni kuwapa wananchi chaguo lao la kidemokrasi walilolichagua katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana.
Uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba mwaka jana ulifutwa na tume ya uchaguzi kwa kile kilichoelezwa kuwa ulikuwa na kasoro. Uchaguzi huo ulifanyika tena Machi 20 mwaka huu na kumpa Dkt Shein ushindi.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE