
Hali ya wasiwasi iliyoanzishwa na
upigaji kura wa Uingereza kuondoka Jumuiya ya Ulaya (EU) imekumba chama
kikubwa cha upinzani cha Leba.
Nusu ya Baraza la Mawaziri la
upinzani linatarajiwa kujiuzulu hii leo likilalamikia jinsi kiongozi wao
Jeremy Corbyn alivyoongoza kampeni ya kura za maoni.
Wa kwanza
kuondoka alikuwa Waziri wa Afya, Heidi Alexander, aliyesema kuwa Bwana
Corbyn hana kipaji cha kushughulikia matatizo yanayokumba Uingereza kwa
wakati huu.
Awali, Waziri wa upinzani wa Mashauri ya Kigeni,
Hilary Benn, aliachishwa kazi kwa kile Bwana Corbyn alidai kuwachochea
wenzake waondoke katika baraza hilo iwapo Bwana Corbyn, atakataa
kuheshimu mswada wa kutokuwa na imani kwake.
Wafuasi wengi wa Leba walipiga kura kwa Uingereza kujiondoa katika Jumuiya ya Ulaya.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment