Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Baada ya miaka mingi ya uhusiano thabiti na
uliokuwa umetawaliwa na upendo usio kifani, Mwenyekiti Mtendaji wa
Bongo5 Media Group Limited, Luca Neghesti na Miss Tanzania 2005 na Miss
World Africa, Nancy Sumari wamefunga ndoa .
Luca na Nancy ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5 wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Zuri.
Wawili hao wamefunga ndoa Ijumaa iliyopita jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu takriban
60 ambao wengi wao ni ndugu na marafiki zao wa karibu. Tunawapongeza kwa
hatua hiyo kubwa kwenye maisha yao. Tazama picha zaidi hapo chini.





Luca akisaini cheti cha ndoa

Nancy akisaini cheti cha ndoa

Ndugu na jamaa wakishuhudia tukio
0 MAONI YAKO:
Post a Comment