
THE CIVIC UNITED front (CUF – Chama Cha Wananchi)
DIRECTORATE OF INFORMATION, PUBLICITY AND PUBLIC RELATION
P.O.BOX 10979 DAR ES SALAAM homepage: www.cuftz.org email: cufhabari2008@yahoo.com
Director: Salim Biman Zantel No. 0777 414 112 / Voda No. 0752 325 227
A/Deputy Director: Mbarala Maharagande Airtel No. 0784 001 408 / Halotel No. 0621 715 795
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Imetolewa leo Tarehe -11/9/2016
Na Julius Mtatiro
SALAMU ZA POLE NA RAMBIRAMBI KUTOKANA NA TETEMEKO LA ARDHI LILILOSABABISHA MAAFA KATIKA MIKOA YA MWANZA,
KAGERA NA GEITA
THE
CIVIC UNITED FRONT (CUF- Chama Cha Wananchi) kinapenda kutoa mkono wa
pole na kutuma salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa wa marehemu
waliopatwa na maafa kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea katika
mikoa ya Mwanza, Kagera na Geita , Kaskazini Magharibi ya Tanzania
karibu na ziwa Victoria. Tetemeko hilo lililosababisha madhara makubwa,
uharibifu wa mali, kusababisha majeruhi na vifo kwa watanzania wenzetu.
Kwaniaba ya Chama Cha CUF napenda kuchukua fursa hii kuwapa pole wale
wote waliofikwa na maafa haya familia, ndugu, jamaa na marafiki wawe na
subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na tunamuomba Mwenyezi
Mungu awapokee marehemu wote awasamehe makosa yao na kuwaingiza katika
ufalme wake wa mbinguni- ameen. Aidha, tunawaombea majeruhi wote
waliofikifishwa katika vituo vya matibabu wapone haraka ili waweze
kurejea katika majukumu yao ya kila siku ya ujenzi wa Taifa letu na
familia zao.
Tunatoa wito kwa watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuwasaidia kwa hali na mali na kwa namna moja au nyingine waathirika wote waliopatwa na maafa haya ili kuendeleza utamaduni mwema wa Umoja, Undugu na Mshikamano kama watanzania. Aidha, tunaziomba mamlaka husika za hali ya hewa kutekeleza wajibu wake ipasavyo ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na majanga kama haya kwa siku za usoni.
Tunatoa wito kwa watanzania wote kujitokeza kwa wingi kuwasaidia kwa hali na mali na kwa namna moja au nyingine waathirika wote waliopatwa na maafa haya ili kuendeleza utamaduni mwema wa Umoja, Undugu na Mshikamano kama watanzania. Aidha, tunaziomba mamlaka husika za hali ya hewa kutekeleza wajibu wake ipasavyo ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na majanga kama haya kwa siku za usoni.
Tetemeko
hilo la ardhi lenye uzito wa 5.7 katika vipimo vya richa limetokea jana
katika eneo la kaskazini magharibi ya Tanzania hasa katika mikoa ya
Kagera, Mwanza, na Geita karibu na ziwa victoria.
Chama
cha CUF katika ibara ya 7(14) inayozungumzia Lengo na madhumuni ya chama
inaeleza kuwa “ kuwalinda (kuwasaidia)......wananchi wanaokumbwa na
maafa na majanga au wale wanaopuuzwa na dola yao hasa wakati wa majanga
makubwa.”
haya ni katika madhumuni ya chama yaliyoainishwa katika katiba yake.
HAKI SAWA KWA WOTE
_________________________________
JULIUS MTATIRO
MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI CUF TAIFA.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment