October 27, 2016



Dkt. Jonas Tiboroha katibu mkuu wa klabu ya Yanga
Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga Dkt. Jonas Tiboroha kwa mara ya kwanza amezungumzia sakata la kuondoka kwake klabuni hapo baada ya kwenda kinyume na uongozi wa Mwenyekiti aliyepo madarakani Yusuf Manji.
Tiboroha ambaye hakupenda kuzungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuondoka kwenye klabu hiyo ya Jangwani mwaka uliopita amesema, imekua ni vigumu kwa watu kufanya kazi na Yusuf Manji kutokana na mwenyekiti huyo kutaka kupindisha baadhi ya mambo kwa makusudi.
Amesema wakati wa utawala wake alitaka kuona kila hatua inafuata taratibu za kikatiba kwa maslahi ya klabu  ya Yanga, lakini msimamo wake ulimponza na kufikia hatua ya kuandika barua ya kujiuzulu.
“Kila mtu anaweza kuwa na sababu zake, kuna wengine waliondolewa wakaambiwa wezi, wengine tuliambiwa tulishindwa kufanya yae kazi, ikawekwa press comference vitu vya ajabu sana vikaongolewa kwamba nawafukuza wachezaji, naingilia majukumu ya kocha lakini nataka nitumie fursa hii kuongea kauli moja, unapokuwa kiongozi wa klabu kubwa kama Yanga na wakati huo ukawa na mwenyekiti ambaye huyohuyo ni mdhamini wa timu kuna changamoto nyingine unaweza kushindwa kuzifanya.”
“Unapokuwa unafanya kazi ya kuajiriwa vitu kama hivi lazima uvitegemee kwasababu utakapokuwa umeshindwa kuelewana na mtu kwasababu ya kitu ambacho ni cha msingi, njia sahihi ni wewe kuondoka ukaacha watu wengine wakaja kufanya vitu anavyovitaka yeye.”
“Hali iliyopo Yanga sasahivi kwa mtu kama mimi ingekuwa ngumu sana kunishawishi kama mtendaji mkuu wa klabu, ningehitaji kuona sababu zinazoeleweka ili nikiulizwa na watu tofauti kama vyama vya michezo, wizara au wanachama niweze kuwa na majibu ya kuwaeleza kwa kitu kinachokuja kwenye klabu na siyo tu kupitisha vitu ambavyo ukiulizwa maana yake ni nini unashindwa kueleza.Sasa haya ni mambo ambayo yapo nyuma ya pazia, na yanapokuwa tofauti unajiuzuli na kuondoka”


0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE