M/Kiti wa chama cha wananchi CUF Prof.Ibrahim Lipumba ameteua wakurugenzi wapya pamoja na manaibu wakurugenzi katika chama hicho ikiwa ni siku moja tu baada ya kutengua baadhi ya kurugenzi ndani ya chama hicho.
Akitangaza kurugenzi mpya mbele ya waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho Buguruni jijini Dar es salaam, Prof.Lipumba amemteua Thomas Malima kuwa Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha, Maftah Nachuma Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, Zainab Mndolwa Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria.
Wengine walioteuliwa ni pamoja na Masoud Mhina Katibu Kamati ya Ulinzi na Usalama, Jaffar Mnete, Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi ambapo wakurugenzi na manaibu wakurugenzi aliowateua baada ya mkutano mkuu wa Juni mwaka 2014 wataendelea na nyadhifa zao.
Kwa Upande wa Jumuiya ya wanawake Cuf Taifa- JUKECUF amemteua Salama Masoud kuwa katibu mkuu wa Jumuiya hiyo badala ya Fatuma Omar Kalembo kuwa na matatizo ya kiafya.
Aidha Prof.Lipumba amemuagiza Mkurugenzi mpya wa Uchumi na Fedha ambaye ndiye katibu wa bodi ya wadhamini aitishe kikao cha dharura cha bodi ya wadhamini ili wapewe taarifa ya Msimamo na Ushauri wa Msajili wa vyama vya siasa kuhusu mgogoro wa Uongozi wa kitaifa ndani ya chama hicho siku ya Jumanne.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment