October 29, 2016

 
 Julius Mtatiro akiwa na Kuli ni #Mmusi_Maimune, kiongozi wa chama cha DA na Kiongozi Mkuu wa Upinzani Afrika ya Kusini. (Kwenye Bunge la Afrika Kusini). na Kushoto ni Mhe. #Nevers_Mumba, Makamu wa Rais wa Zambia (2003-04) na kwa sasa ni kiongozi wa chama Kikuu cha upinzani nchini Zambia (MMD).

" Maono yetu ni kuiona Afrika yenye demokrasia pana zaidi na maendeleo yanayopimika. Moja ya maazimio ya Mkutano huu itakuwa ni kuunda Oganaizesheni ya Kudumu itakayounganisha vyama vyote mbadala vilivyoko barani Afrika ili kuhakikisha kuwa mabadiliko ya Waafrika yanasimamiwa kwa umoja thabiti".

JSM,
SA.


Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya The Civic United Front, Mhe. Julius Mtatiro yuko nchini Afrika ya Kusini kwa safari ya kikazi ya siku 5 akikiwakilisha chama.
Mhe. Mtatiro amealikwa na taasisi za kidemokrasia za FPD na ADI za Kusini mwa Afrika na ataviwakilisha vyama vya upinzani vilivyoko Afrika ya Mashariki na ukanda wa SADC.
Katika Mkutano huo Mhe. Mtatiro amepewa fursa ya kuwasilisha mada juu uzoefu wa changamoto zinazovikumba vyama vya Upinzani Afrika Mashariki. Mada hiyo itawakilishwa mbele ya viongozi mashuhuri wa vyama vya upinzani walioko Kusini mwa Afrika wakiwemo viongozi wakuu wa DA ya Afrika ya Kusini, MDC ya Zimbabwe n.k.
Mhe. Mtatiro pia amepata mwaliko maalum wa Mazungumzo ya faragha na kiongozi wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini Afrika ya Kusini (DA), mhe. Mmusi Maimane, ambapo watazungumzia juu ya uimarishaji wa uhusiano wa kidugu uliopo kati ya DA na CUF ikiwa ni pamoja na kupanga Programu za kujengeana uwezo kati ya vyama hivi viwili.
Pamoja na mambo mengine mhe. Mtatiro pia atakutana na wakuu wa taasisi za FPD na ADI kwa ajili ya mazungumzo maalum ya uimarishaji na ukuzaji wa mahusiano ya kimataifa kati ya CUF na taasisi za Kidemokrasia za Kusini mwa Afrika.
Wakati Kiongozi wa CUF akiendelea na majukumu yake ya kikazi kitaifa na kimataifa, Chini ya ulinzi mkali wa Jeshi la polisi aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF Prof. Lipumba ameungana na baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Buguruni kufanya usafi jambo ambalo ñi nzuri kwa ustawi wa mazingira bora na kulinda afya kwa wakazi wa eneo hilo, wafanyabiashara na wateja wanaofika sokoni hapo. Eneo la buguruni ni hatarishi pindipo mazingira yasipokuwa salama kwa usafi kusababisha magonjwa ya mlipuko na kipindupindu.
Ni ushauri wetu kwa Lipumba na wenzake kuanzisha NGO ya kitaifa itakayojishughulisha na masuala ya usafi wa mazingira na upandaji miti ili kusaidiana na serikali ya awamu ya tano ambayo amejenga nayo mahusiano mazuri ya kuisaidia kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM -2015-2020. Ni matarajio yetu kuwa kama ataufanyia kazi ushauri huu waziri mhe January Makamba na Mhe Rais Magufuli watampa ushirikiano mkubwa. Huku kwenye siasa angeheshimu na kubaki na msimamo wake wa kung'atuka na kusutwa na dhamira yake na kukaa pembeni. Jamiii ya watanzania na wanachama wa CUF waliowengi wamepoteza imani nae kwa kiwango kikubwa.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma,
The Civic United Front (CUF).
29 Oktoba 2016.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE