October 03, 2016



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,jana tarehe 03 Oktoba, 2016 amemteua Prof. Lawrence Mujungu Museru kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Lawrence Mujungu Museru umeanza jana tarehe 02 Oktoba, 2016.

Kabla ya Uteuzi huo Prof. Lawrence Mujungu Museru alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

03 Oktoba, 2016

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE