Baada
ya mashabiki wa Simba kuvunja viti vya uwanja wa taifa katika mchezo wa
Simba na Yanga uliopigwa Jumamosi na kumalizika kwa sare ya goli ya
moja kwa moja, serikali kupitia kwa Waziri wa Michezo, Nape Nnauye Imepiga marufuku uwanja wa taifa kutumika na timu za Yanga na Simba.
Waziri Nape amefanya maamuzi hayo baada ya jana Jumapili kufanya ziara katika uwanja wa taifa kushuhudia uharibifu wa viti uliotokea juzi Jumamosi .
Amesema kutokana na tukio ambalo limejitokeza, kuanzia sasa michezo ya timu hizo haitaruhusiwa kufanyika katika uwanja huo hadi pale ambapo serikali itawaruhusu.
“Uwanja
huu hautatumika kwa Yanga na Simba mpaka pale tutakapoamua vinginevyo
hapo baadae, hawatatumia uwanja huu watafute viwanja vingine, sababu
hapa kuna pesa za walipa kodi, kuna pesa za watanzania.
“Wanaotakiwa
kutumia uwanja huu ukiwa mzuri kama ulivyo ni wengi kuliko Yanga na
Simba, wapo wengine ambao ni wastaarabu wanaweza kutumia uwanja huu,” aLIsema Waziri Nape.
Maamuzi
mengine ni Simba kutakiwa kulipia gharama ya viti 1,781
vilivyoharibika, Simba haitapata mgao wa mchezo hadi walipe gharama za
uharibifu, kamera za CCTV zitafungwa uwanja mzima na Yanga itatakiwa
kulipa gharama ya mageti manne ya upande wa mashabiki wake yaliyovunjwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment