
Aliyekua mgombea Ubunge wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Jimbo la
Mvomero mwaka 2015, Mchungaji wa kanisa la Assemblies of God, Oswald
Mlay na wenzake wawili wameamua kurejea chama cha mapinduzi (CCM) kwa
kile walichodai kuridhishwa na kasi ya utendaji kazi wa Rais Dkt. John
Magufuli.
Akizungumza na katibu wa mkoa wa chama cha mapinduzi mkoa, Kulwa
Milonge, Mchungaji huyo amesema kuwa kwa ridhaa yake mwenyewe ameamua
kurejea chama cha mapinduzi kwa kuwa kina sera nzuri na
zinazotekelezeka.
“Ninawashukuru kwa kunipokea, mimi ni mfanyakazi nakipenda chama na
nina nguvu na ntashilikiana na wananchi wenzangu wa chama cha mapinduzi.
Kwakweli niseme Rais Magufuli anafanya kile nilichokuwa nakitaka vile
nilivyokuwa navitaka amevifanya na vimeshapitiliza. Kwahiyo sina sababu
ya kuwa mnafki kuwa mpinzani na kumuacha mtu kama Rais Magufuli awe peke
yake. Kwahiyo narudi nyumbani naomba mnipokee. Katibu ntafanya kazi
popote utakapoona nafaa kwa mawazo ushauri kwaajili ya chama chetu,”
alisema Mlay.
Wengine waliohamia CCM ni Paul Mboji na Patrick Ambi
Hivi karibuni, Mbunge wa zamani wa NCCR Mageuzi, Moses Joseph Machali
alihamia CCM huku naye akidai kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais
Magufuli.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment