January 17, 2017

Image result for zitto kabwe 

 Kufuatia sintofahamu ya uwepo wa janga la njaa nchini au lah! huku mvutano wa jambo hilo ukiendelea kuwa mjadala mkubwa nchini kwa sasa, Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe ametoa sharti la kujiuzuku endapo Serikali itamuonesha hifadhi ya chakula katika ghala la Taifa

KAULI YA ZITTO:

"Serikali ya CCM ikinionyesha tani 1.5m za chakula kutoka Hifadhi ya Taifa ya Chakula ambazo inataka kusambaza najiuzulu Ubunge mara moja. 
Narudia, mpaka Oktoba 2016 kulikuwa na nafaka tani 90,400 tu Hivi kwenye maghala yote ya NFRA.
Tunashukuru kuwa Hivi sasa ajenda ya tishio la njaa inapata majawabu na matamko. Ndio wajibu wa vyama vya siasa. Kuibua masuala muhimu kwa nchi yetu.
Nimesikia Mwenezi wa CCM ameongea na waandishi Leo. Natarajia ndugu Ado Shaibu atamkaribisha mwenzake ulingoni"

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE