Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Mabingwa wa Kombe la Shirikisho
nchini Simba SC, Zakaria Hans poppe amekanusha timu yake kuwasajili
wachezaji Aishi Manula, John Bocco, Shomari Kapombe pamoja na Emmanuel
Okwi na kusema taarifa hizo ni za uongo.
Hans poppe amebainisha hayo baada ya kuenea kwa tetesi kuwa timu hiyo
imeshawasajili wachezaji hao baada ya msimu 2016/2017 kuisha hivi
karibuni.
“Ni uongo kusema kuwa sisi tumeshaingia mkataba na mchezaji yoyote maana
hadi sasa mikataba ya wachezaji bado haijamalizika, tukisajili mtu sasa
itakuja kuwa kama suala la Kessy ambalo tuliwaambia Yanga lakini
wakajifanya wajuaji, matokeo yake wametema milioni 50 tena kwa huruma
yetu” alisema Poppe.
Pamoja na hayo, Hans poppe amesema kwa sasa hawezi kusema chochote kama wameanza mazungumzo na wachezaji hao wanaotajwa zaidi.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment