Viongozi wa vyama vya siasa vya
upinzani wamelaani kitendo cha serikali ya mkoa wa Kilimanjaro cha
kuzuia uwanja wa Mashujaa kutumika kwa ajili ya ibada ya kuaga mwili wa
marehemu Philemon Ndesamburo, na kudai kuwa kililenga kuendeleza chuki
ya kisiasa.
Katika hatua nyingine, wameshangazwa
na CCM kutokuwa na muwakilishi katika ibada ya kuuga mwili wa Ndesamburo
aliyefariki dunia wiki iliyopita wakati akipatiwa matibabu katika
hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa
amesema kitendo hicho kimelenga kudhibiti demokrasia. “Nawapongeza kwa
maandalizi haya. ila kwa hili inaonyesha jitihada za kudhibiti
demokrasia zinaendelea, watu hawa ni wa kuwasamehe bure.
Naye mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa
Pwani, Fredrick Sumaye amesema “Hata njia za kupitisha maiti nazo
zinalindwa hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai, wananchi
hatutaweza kuwaonea muda mrefu. Ila mbegu ya amani aliyoipanda
Ndesamburo itaendelea kuzaa aliyoyasimamia.”
Wakati akitoa salamu hizo, Mwenyekiti
mwenza wa UKAWA, James Mbatia amesema kitendo cha viongozi wa CCM
kutohudhuria kwenye ibada hiyo si cha kiungwana kwani kinalenga kugawa
wananchi kwa misingi ya vyama.
“Walichofanya leo sio cha kiungwana,
watanzania tusikubali kugawanyishwa kwa misingi ya imani wala vyama,
sijauona uwakilishi wa CCM, tuwasamehe na mimi nimewakilisha CCM wote
hapa ili tulete amani ya mzee Ndesa.Ndesamburo alikuwa analeta watu wote
pamoja, lakini leo hata njia za kupitisha mwili wake nazo zinalindwa
hizi chuki tukiacha zijengwe hatutakua hai,” amesema.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti CUF
Severina Mwijage wakati akitoa salamu za rambirambi amesema
amesikitishwa na kitendo cha kuzuiwa uwanja kwani marehemu Ndesamburo
alishiriki kuujenga uwanja huo.
“Siasa za sasa hivi ni hatari, za
kupandikiza watu chuki ni mbaya sana, na mimi naomba niongezeee wenyewe
wanajua chuki ndio chama chao kitakachosaidia kuchukua dola, sisi
tunachaguliwa na wananchi tunajua matatizo ya wananchi, aelewe yule
anayewachonganisha itakuaje yeye ambaye aliyemchagua atakuja na kuondoka
na yeye atabaki katika mkoa na watoto wake wanaishi na wananchi,”
amesema.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment