August 18, 2017

Benki ya TIB Corporate imeweza kushiriki jukwaa la biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga ambapo kutoa fursa za namna ya benki hiyo inavyoendesha shughuli zake hapa nchini.
Wakielezea fursa hizo mbalimbali katika  Mkoa wa Tanga, benki inajiweka sawa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wana Tanga.
“Tunambua kuwa maendeleo yoyote yale ya kibiashara na viwanda yanahitaji uwezeshwaji wa kifedha (bank facilities). TIB Corporate Bank  inatoa Huduma mbalimbali kutokana na mahitaji ya Mteja.hii ni pamoja na akaunti mbalimbali za kwa makampuni na Watu binafsi, mikopo ya aina mbalimbali ya muda mfupi na muda wa kati, dhamana za kibenki ( bank guarantee), ununuaji na uuzaji wa fedha za kigeni, uwekezaji katika hati fungani,(treasury bills & Bonds).
Ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni (cash management ) pamoja na ulipaji wa mishahara kwa Njia rahisi na haraka. Huduma zetu hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha Mteja anafurahia mahusiano yake na benki. Pia huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha zaidi” walieleza TIB.

Mkurugenzi wa Mkuu wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege akizungumza wakati wa Jukwaa la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga

 
 Waziri wa Habari akiwa katika picha ya pamoja na wadau hao
 
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate ,Theresia Soka akizungumza wakati wa Jukwaa hilo

Waziri wa Habari akiwa katika picha ya pamoja na wadau hao

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE