June 27, 2018

 Wakazi wa Kata ya Rudewa wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wakiwa makini kumsikiliza Mbunge wa Jimbo hilo Mbraraka  Ba Waziri wakati alipokua akifanya mkutano na wananchi hao akiskiliza kero na kutoa utatuzi kwa baadhi ya kero hizo

 Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akihutubia wakazi wa vijiji na kata ya Rudewa wakati wa mkutano na wananchi hao alipokua akisikiliza kero na kutoa utatuzi wa kero hizo ikiwemo katika sekta ya Afya, Elimu na Maji.

Diwani wa kata ya Kimamba  Pendo Mpoto akihutubia wananchi wa kata ya Rudewa wakati wa mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri alipoku akiongea na wananchi kuhusu matatizo mbalimbali ya nayo wakabili sambamba na kutoa msaada wa vifaa kwaajili ya utatuzi wa kero za Maji Elimu na Afya

 Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akimpa mkono diwani wa kata ya Rudewa Subiri Joseph wakati akikabidhi mradi waujenzi wa kisima cha mita 100 kwaajili ya kutatua kero ya maji katika kijiji hicho kulia ni katibu wa CCM wilaya ya Kilosa Aziza Juma   kushoto Hassan Mkopi Mwenyekiti wa Halmahauri wilaya ya Kilosa pamoja na viongozi mbalimali wa CCM na serikali.

Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri akikabidhi diwani wa kata ya Rudewa Subiri Joseph moja ya mfuko wa simenti kama mfano  kwaajili ya ujenzi wa madarasa ya shule katika kijiji cha Rudewa Kata ya Rudewa Walayani Kilosa ambapo alitoa msaada wa simenti 200 kwaajili ya shughuli hiyo.
Mbunge wa jimbo la Kilosa Mbaraka Ba Waziri ametoa msaada wa ujenzi wa kisima kikubwa cha mita 100 ambacho kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya vijiji viwili katika kijiji cha Rudewa kilichopo kata ya Rudewa wilayani Kilosa  ambapo ujenzi wake umeanza mara moja, kutokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kuwa tatizo sambamba na ahadi ya  ujenzi wa kituo cha afya kwaajili ya huduma ikiwemo ya wajawazito pamoja na watoto huku tayari akiwakilisha  bati 120 waajili ya ujenzi wa kituo cha afya simenti 200 kwaajili yakujenga vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Rudewa katika wilaya ya Kilosa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE