
Msanii muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ataiwakilisha Tanzania kwenye
meza ya majaji wanne waliotangazwa na waandaaji wa shindano la East
Africa’s Got Talent 2019.
Majaji wengine watatu waliotangazwa jana watakaosimamia shindano hilo
kwa msimu wa kwanza ni mtangazaji wa runinga kutoka Kenya, Jeff
Koinange, Gaetano Kagwe (Uganda) na Contact Makeda (Rwanda).
Shindano hilo litaanza kuonyeshwa mwezi Agosti 4, mwaka huu kwenye vituo mbalimbali vya runinga hapa Afrika Mashariki.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment