Ray C akiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu alipokwenda kumtembelea
Msanii wa Kizazi Kipya hapa nchini ,maarufu kama Bongo Flavour, Bi Rehema Chalamila anaejulikana zaidi kama Ray C,m jana mchana amefika Ikulu ya Dar-Es-Salaam kumshukuru Rais Jakaya Mrisho
Kikwete kwa msaada mkubwa wa matibabu yake ambayo yanafanyika jijini
Dar-Es-Salaam
Ray C
amefika Ikulu akiongozana na mama yake mzazi Bibi Margareth Mtweve
ambaye pia amemshukuru Rais Kikwete kwa msaada huo mkubwa ambao
umesaidia kurudisha hali ya kawaida ya Ray C.
Rais amempongeza Ray C kwa kukubali hali yake ya kiafya na hatimaye kukubali kupata matibabu ambayo bado anaendelea nayo chini ya uangalizi maalum.
Rais
amemtaka mwanamuziki huyo kufuata masharti ya madaktari ili aweze kupona
kabisa na hatimaye kurudia hali yake ya mwanzo na kurejea katika
shughuli zake za kujitafutia kipato na maisha.
Kwa vile Ray C
bado yuko katika matibabu, hatutaweka wazi sehemu anayotibiwa hadi
atakapokuwa tayari kabisa kurudi katika shughuli zake rasmi hivyo
tunaomba jamii impe ushirikiano huo na kuheshimu taratibu zake za
matibabu ili hatimaye aweze kupona kikamilifu.
“MWISHO”
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Ikulu-DSM
10 Desemba, 2012
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Ray C (wa pili kulia), Mama
yake mzazi Ray C, Bibi Margareth Mtweve (kushoto) na kulia ni Sarah
Mtweve Dada yake Ray C.
PICHA NA
Picha na Freddy Maro
0 MAONI YAKO:
Post a Comment