
Mfalme na wanae
Siku ya jana tarehe 24/4 mfalme wa Rhyme Tanzania Mfalme Sele, aliadhimisha umri wake wa kuzaliwa. Hakuipitisha bure, tazama alichokisema na kukupa zawadi wewe mdau wake.
Jana nimetimiza miaka 37, asanteni kwa kunitakia kheri/furaha na dua zenu njema kwangu kwa Mungu katika siku yangu ya kuzaliwa. Katika ujio huu wa umri na siku zangu za kuishi zinapungua! Kama tunasherekea siku ya kuzaliwa tukumbuke kuna siku ya kufa vilevile, siku ya kuzaliwa iwe changamoto kwetu sote kwa kutathimini sababu za uwepo wetu duniani na kusudio la muumba wetu kutuumba wanadamu, na si wanyama, ndege, wadudu au samaki. Lakini tujifunze kuwa maisha(kuishi) ndio zawadi kubwa pekee aliyotupa Muumba wetu. Tuyatunze maisha yetu na ya wengine kwa kutenda HAKI bila kikomo. HAKUNA ALIYEMKAMILIFU CHINI YA JUA, DUNIA AIHITAJI WAKAMILIFU INAHITAJI WATU WA KWELI. Zawadi yangu kwenu katika ujio huu wa umri ni huo wimbo DINI TUMELETEWA ..... MUNGU AWABARIKI SANA.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment