
Agnes Masogange
Jeshi la Polisi litapeleka
askari wake Afrika Kusini kuwahoji washiriki wa video za wasanii wa
muziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald ‘Masogange’ na mwenzake Melisa
Edward waliokamatwa nchini humo na dawa za kulevya.
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya,
Godfrey Nzowa aliliambia gazeti hili kwa simu jana kuwa watawapeleka
polisi kuwahoji na wanaamini wahusika watawaeleza wahusika wa mzigo huo.
Wasichana hao walikamatwa kwenye Uwanja wa Ndege
wa Oliver Tambo nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania wakiwa na kilo
150 za dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine.
“Tutawapeleka askari wetu kuwahoji, tumekwishaanza uchunguzi wa hili...wote watakaohusika katika hili tutawakamata, lakini tunakwenda polepole hatua kwa hatua kuhakikisha tunawanasa wahusika sahihi,” alisema Nzowa.
Naye Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere, (JNIA), Moses Malaki alieleza kushangazwa na kiasi kikubwa
kupitishwa kwenye uwanja huo licha ya kuwa wapo watu wenye dhamana ya
kuangalia usalama.
“Sitaki kusema tutafanya nini, lakini ninachotaka
kukwambia ni kwamba uchunguzi umeanza na suala zima tumewaachia polisi
na sisi tutatoa ushirikiano kwa kila hatua watakayotutaka, lazima
kukomesha hili.
“Tutaangalia nani walikuwa zamu siku hiyo,” alisema Malaki.
Chanzo Mwananchi
Chanzo Mwananchi
0 MAONI YAKO:
Post a Comment