Msanii
wa Hip Hop Bongo,Elibarik Emaniel‘Nay wa Mitego amefunguka kuwa kama
akifariki dunia hataki aundiwe kamati za ajabu ajabu za wasanii wenzake
wa muziki huo kwani wengi wao hutumia kamati hizo kama mitaji kwa
kutafuna pesa za rambirambi.
Aidha amefunguka kuwa ameamua kuzungumza hivyo baada ya kupokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wasanii,baada ya kuwadis kupitia ngoma yake aliyoiachia ya Salaam Zao kuwa waliochukua pesa za rambirambi za Ngwea warudishe hata kimya kimya kwani muda wanao.
‘Zipo nyingi zingine za vitisho,nitazipost zote watu wangu mujue leo nimeanza na hiyo…! Ukweli unauma sana siogopi vitisho vyenu…pelekeni hela za marehemu hata kimyakimya bado nafasi mnayo,,,mi nikifa sitaki kamati za kwenye msiba wangu maana watu wanafanya misiba yetu mitaji yao’alisema Nay.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment