
Chid Benz akiwa na DJ Fetty wa Clouds fm
Rapper
Chidi Benz leo kwa mdomo wake mwenyewe amekiri kuwa alikuwa akitumia
madawa ya kulevya kwa miaka mingi. Chidi amefunguka leo kwenye kipindi
cha XXL cha Clouds FM.
Alisema
japo hakwenda Nairobi kwaajili ya rehab, mazingira yalimlazimu kutafuta
tiba ili aondokane na madhara ya madawa hayo. Alieleza kuwa alipofika
jijini Nairobi alikuwa akitakiwa kufanya show nyingi na mwandaaji
alimuuliza kama kuna kitu atahitaji ili awezE kufanya show vizuri.
“Nikamwambia
Yeah kuna vitu ntavihitaji,” alisema Chidi. “Nikamwambia ‘mimi bana
kuna vitu ninavyovitumia nikikaa 20 minutes bila hivyo vitu ni noma
nachanganyikiwa na akili tena sina, kwahiyo sijui tutafanyaje’.
Akaniambia
‘mimi ntapataje hivyo vitu Chidi na Nairobi ni gharama sana.
Nikamwambia ‘mimi pia nina wazo jingine kuna mtu alinitonya kwamba kuna
kitu kinaweza kikafanyika na pesa Fulani, pesa nyingi kama milioni 15,
16 hivi za kibongo.
Akaniambia
kikifanyika hicho maanake vinavyofolewa kabisa hivyo vitu vilivyokuwa
vinanifanya niwe hivyo. Akaniambia ‘hiyo naijua lakini ni process, ndio
maana dunia nzima haifanyi’. Nikamwambia ‘mimi nafanya kwasababu
nilishakutwa na vitu vingi mimi ntafanya.”
Chidi anasema hela hiyo ilipatakana na wakapanga kwenda kufanya mchakato huo wa kuonana na daktari ili kutibiwa.
“Kwahiyo mimi sijaenda rehab na wala sijanywa zile methodone sijui watu wanasema watu wanywe methodone.”
Amesema dawa aliyotumia inanunuliwa na mtu huchomwa kama mgonjwa wa kawaida.
“Yenyewe
inakusafisha wewe pale ambapo ulikuwa ukivuta inakukaa then baada ya
dakika kadhaa pakikauka panakuwa pakavu ni kama ile sehemu inakuwa
mbichi wewe ukivuta. Huna hela lakini huvuti panakuwa pakavu, pakikauka
ndio unachanganyikiwa unaanza sasa kuona alosto lakini kama ukiendelea
kuvuta panakuwa pabichi unaendelea.
So
yenyewe inaenda kama mapovu, ni kama sabuni inaenda inakusafisha pale
kote panabaki empty. Kwahiyo ni wewe sasa uamue tena kuvuta tena au
uache kabisa. Lakini mimi nilienda kusafishwa pote, inakuweka unakuwa na
power, inakupa akili, uso rangi, mwili unaanza kubadilika.”
Anasema kabla ya kupata tiba hiyo alitakuwa kusaini karatasi kadhaa kuthibitisha kuwa amekubali kupewa dozi.
“Mama yangu pia alikuwa anajua, nilimwambia kwamba mimi bana inabidi nitibiwe.”
“Niko
fresh, niko healthy, nakula vizuri, naishi vizuri, nafikiria vizuri na
nimecalm down,” alisema Chidi kuelezea hali yake ya sasa
Chidi
amekiri kuwa alianza kutumia madawa ya kulevya muda miaka mingi
iliyopita lakini ilikuwa ngumu wengi kujua kwasababu alikuwa akiutunza
vizuri mwili wake.
“Naoga
vizuri, nakula vizuri, nafanya mazoezi daily, gym daily, kwahiyo hata
nikivuta hayanitibui kitu lakini yalikuwa yananijaza tu anger ndani,
chuki na ule unoma unoma.”
0 MAONI YAKO:
Post a Comment