November 27, 2013


Stori Kutoka Global Publishers
KUNA mengi ya kushangaza duniani lakini hili la kijana Hamad Issa (32) kunaswa faragha na bibi kizee Adela Mkalau (80) linaongeza rekodi ya mambo yanayoshangaza, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu.
 
 Hamad Issa (32) akiwa amejilaza kitandani kwa bibi Adela Mkalau (80).
Tukio hilo la kustaajabisha limetokea mwishoni mwa wiki iliyopita, nyumbani kwa bibi huyo, Yombo –Buza, jijini Dar es Salaam ambapo wajukuu wa bibi huyo ndiyo waliomnasa.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, wajukuu wa bibi huyo walifedheheshwa na kitendo hicho hivyo kuwawekea mtego na kuwanasa kisha kumfikisha Hamad katika Kituo cha Polisi Chang’ombe kwa tuhuma za ubakaji.
Bibi Adela Mkalau (80) akiwa katika pozi.
BIBI: SIJABAKWA
Katika kutafuta uhakika wa madai ya wajukuu hao, polisi wa Chang’ombe waliagiza bibi yao aitwe ili athibitishe madai hayo wakati upelelezi mwingine ukiendelea.
Sosi wetu alisema kuwa bibi aliwaacha hoi polisi baada ya kufika kituoni hapo na kukataa maelezo ya wajukuu zake, huku akisisitiza hakubakwa bali walikubaliana na Hamad.
Baada ya bibi huyo kuondoa utata, polisi walikubali kumuachia Hamad kisha wajukuu wakafunguliwa kesi ya kushambulia na kudhuru mwili iliyoandikishwa kituoni hapo kwa jalada namba CHA/RB/10629/2013.
Hamad Issa akiwa kitandani, pembeni kulia ni bibi Adela Mkalau.
BIBI NA RISASI
Risasi Mchanganyiko lilifunga safari hadi nyumbani kwa bibi huyo na kuzungumza naye kuhusu tukio hilo ambapo alisema: “Sijabakwa na nimekasirishwa sana kwa kitendo cha kumpiga kijana wangu. Wawe na heshima kwa babu yao. Sisi tunapendana, kwa nini wanatuingilia?”
Alisema: “Siku hiyo Hamad wangu alikuja nyumbani kwangu tangu mapema. Nikaandaa chakula cha jioni, tukala pamoja kisha tukalala.
“Tukiwa usingizini, nikasikia mlango unagongwa. Kwenda kufungua, wajukuu zangu wakaingia na kuanza kumpiga Hamad na fimbo na magongo, wakisema eti amenibaka. Hamad atanibakaje? Kwani mimi ni mtoto mdogo?
“Isitoshe wanamfahamu vizuri sana Hamad. Nipo naye  mwaka mmoja na nusu sasa, leo inakuwaje wanajifanya hawamjui? Siku hizi mambo yamebadilika. Mdogo anaweza kumpenda mkubwa na mkubwa akampenda mdogo. Hakuna kosa.”
Adela Mkalau akiwa kwa bibi.
MSIKIE DOGO
Mwandishi wetu alikwenda nyumbani kwa Hamad ambapo alimkuta akiwa hoi kitandani kwa majeraha ambapo alisema: “Ni kweli bibi ni mpenzi wangu... na wale wajukuu zake wananifahamu vizuri sana. Wamenipiga sana, eti nimembaka bibi yao. Siyo kweli. Sisi ni wapenzi.”
Alipoulizwa anajisikiaje kuwa kwenye uhusiano na kikongwe huyo, alijibu: “Hata mimi nashangaa sijui imekuwaje nikampenda. Nimejikuta nipo kwenye uhusiano naye na kwa kweli tunapendana sana.”
WAJUKUU WANASEMAJE?
Mmoja wa wajukuu wa bibi huyo, Margaret Cheba, akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo alisema bibi yao amewadhalilisha sana na wanaona aibu kupita mitaani kwa kitendo cha kutembea na Hamad.
“Hili jambo limetufedhehesha sana sisi wajukuu zake halafu hata kimila ni tatizo, hairuhusiwi kabisa. Mbaya zaidi, bibi yetu ni mgonjwa. Anasumbuliwa na moyo... sio wa kufanya kitendo kama kile kabisa na sisi ndiyo tunamsaidia lakini inashangaza polisi wametubadilikia kabisa,” alisema Cheba.

Related Posts:

  • VIKOSI VYA YEMEN KIHOUTH MJINI SANA'A    Wanamapinduzi wa Kishia wa Ansarullah wa nchini Yemen wamepigana na vikosi vya serikali huko Sana'a mji mkuu wa nchi hiyo. Watu walioshuhudia wamesema kuwa, sauti za risasi na milipuko kadhaa zimesikika huko… Read More
  • New Vide: K-Cee -Turn By Turn      Moja ya wanamuziki wanaofanya poa sana nchini Nigeria na Africa kwa jumla ni huyu jamaa anaitwa K-cee. hapa nakupa firsa ya kuitazama video yake mpya kabisa        &… Read More
  • ULAYA WAWAPIGIA MAGOTI WAARABU MAPAMBANO YA UGAIDI Mawaziri wa nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels kukiwa na wito ushirikiano wa karibu zaidi kati ya Ulaya na ulimwengu wa Kiarabu katika kukabiliana na makundi ya itikadi kali. Mkuu wa Sera za Nje wa Umoj… Read More
  • IRAN YALAANI MAUAJI YA WANACHAMA WA HIZBULLH   Mohammad Javad Zarif Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imelaani vikali mauaji ya wanachama sita wa Harakati ya Mapambano ya Lebanon Hizbullah yaliyofanywa na utawala haramu… Read More
  • WANAFUNZI WAPINGA UNYAKUZI WA ARDHI    Polisi nchinikenya katiika mji mkuu Nairobi leo imewafyetulia gesi ya kutoa machozi wanafunzi wa shule ya msingi waliokuwa wakiandamana kupinga unyakuzi wa ardhi waliyokuwa wanatumia kama kiwanja cha kuchez… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE