February 06, 2014

 

Kampuni ya Visual Unity Global yaingia mkataba na Clouds Media Group ilikuwezesha jamii kuona matangazo Ya redio kwa njia ya video kupitia kwenye mitandao.Visual Unity Global yaendelea kupanua huduma zake za vuMobile baada ya kusaini mkataba mpya barani Afrika na kampuni ya nchini Tanzania ya Clouds Media Group.Lengo la uhusiano huu likiwa ni kuwezesha jamii kuweza kuona matangazo ya redio kwa njia ya video kupitia kwenye mitandao mahali popote, muda wowote na kukitumia kifaa chochote.Mkurugenzi Mtendaji wa Visual Unity Global,Tomas Petru,alisema: “Kwa kushirikiana na Clouds Media tutasaidia kukua kwa haraka njia ya kupata matangazo ya redio kwa njia ya mtandao nchini Tanzania.”Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga,alisema kuwa “Ushirikiano huo na Visual Unity Global utasaidia kuleta na kukua kwa teknolojia ya kisasa nchini Tanzania ili kuweza kuwanufaisha wateja na wasikilizaji wetu.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE