
Rapper huyo aliyejitoa/ondolewa kwenye label hiyo wiki iliyopita aliachia wimbo mpya uitwao ‘Usiende Mbali’ aliomshirikisha Jux na kutayarishwa na AM Records na Jumatatu hii B’Hits wameachia wimbo wake mwingine mpya uitwao ‘Nishike’. “Mimi hii nyimbo sina taarifa nayo sasa sielewi sababu mimi nilishasema nimemaliza nao na nyimbo tayari nilishafanya sehemu nyingi kwahiyo hii siitambui,” M-Rap ameiambia Bongo5.
“Sawa ni yangu lakini hapo mwanzo walikataa kunipa mimi hiyo nyimbo sababu ni nyimbo ambayo mimi nilikuwa naiulizia itoke, kwahiyo mimi nilishaamua kugive up nikasema naendelea na mambo yangu mengine ilimradi tu nifanya kitu kingine kizuri,” ameongeza.
M-Rap amesema hatofanya chochote kuhusu wimbo huo kwakuwa hautambui.
Bongo5
0 MAONI YAKO:
Post a Comment