April 07, 2014

Baada ya kuweka audio clips za hao mabiniti wakilalamika na kuomba msaada ndipo nilipo amua kuanzisha campaign ili kuwasaidia mabinti hao walioko MACAU. Nilijaribu kwa hali na mali kutafuta mawasilano ili kujua wako wapi na kama habari hizi ni za ukweli. Nilibahatika kuongea na baadi ya watu wanao ishi huko na wakanihakikishia kwamba habari hizo ni za kweli na walinihakikisha kwamba kuna mabinti wadogo sana wanaotumiwa katika biashara hiyo haramu  na wanahitaji msaada haraka iwezekanavyo ingawa wanaogopa kutokana na vitisho wanavyopewa na hao wanaojiita  mabosslady au mama zao. Baada ya hapo ndipo harakati za kuwasaidia zilipo anza na kwa kushirikaina na kaka yangu KWAME tukawasiliana na shirkia la IOM (International Organization for Migration) ambao ndo mara nyingi husaidia watu wenye matatizo kama haya kurudi nyumbani wakatushauri cha kufanya so tukawasiliana na police wa MACAU na kuwaelezea tatizo zima na ndipo jana Jumamosi 5 April 2014 walifanikisha zoezi hilo kama inavvyo repotiwa hapa chini kwenye taarifa ya habari ya TDM ENGLISH NEWS ya MACAU:
 

Natoa wito kwa Serikali kupitia wizara yake husika kuliangalia kwa ukaribu hili suala na kuweza kuwaelimisha mabinti huko nyumbani juu ya mambo haya na athari zake. Yaelekea wengi wanapelekwa nchi za watu bila kuelimishwa vizuri au bila kuwa na ufahamu wa nini haswa wanaweza kukutana nacho huko. Tuna penda kuishukuru Serikali ya Macau kupita jeshi lake la Polisi kwa kuweza kuwafikisha katika vyombo vya sheria wahusika wa biashara hii harua ya Human Trafficking.
 
.

Related Posts:

  • Ancelotti atimuliwa Bayern   Kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti amefutwa kazi leo kufuatia mwanzo mgumu wa msimu wa 2017/18 yakiwemo matokeo ya jana usiku ambapo timu hiyo ilikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa PSG. Mkurugenzi … Read More
  • Unique Sisters warudi kwako wewe    Wasanii wakongwe kwenye game ya muziki ambao ni ndugu wa familia moja Unique Sisters, wamesema wamerudi rasmi kwenye game, kutokana na maombi ya mashabiki na kuachia kazi yao mpya kwa ajili yao inayoitwa '… Read More
  • Mama yake Hayati Samuel Sitta Alipoikaribisha Tigo Fiesta Tabora   Kama ilivyo kawaida ya FIESTA, huambatana na matukio mbalimbali ya Kitaifa, Kwa mkoa wa Tabpora watasherehekea Fiesta siku ya Ijumaa 01 Oct .Geah Habib alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa Hayati Spika wa B… Read More
  • Official Video: Madee ft Nandy - Sema    Madee anatualika hapa kuitazama Video mpya ya wimbo wake wa Sema aliomshirilisha Nandy       … Read More
  • Mbowe Anyang'anywa Gari Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kimesikitishwa na hatua ya uongozi wa Bunge la Tanzania ya kulichukua gari la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe alilokuwa akilitumia kwa sh… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE