May 30, 2014


Baadi ya jamii afrika huoza watoto wao wadogo kwa sababu za kifedha
Umoja wa Afrika umeanzisha kampeini kabambe barani Afrika kusitisha ndoa za watoto wadogo.
Kampeini hiyo ilizinduliwa mjini Addis Ababa katika makao makuu ya umoja huo .
Wataalamu wameonya kuwa ndoa za watoto wadogo zinakatiza ujana wa wasichana zaidi ya milioni kumi na saba, au mmoja kati ya wasichana watatu barani Afrika.
Inakisiwa kuwa asili mia tisini ya nchi zinazoathiriwa na ndoa hizi ni za Afrika
Watetezi wa haki za watoto, wanasema kuwa ndoa za watoto zinakiuka haki za msingi za wasichana kama vile elimu kwasababu wakiolewa wanalazimishwa kuacha shule na kuwahudumia waume zao.
Pia kuna hofu kubwa za kiafya kwa kila msichana mwenye umri mdogo anayepata mimba.
Baadhi wanasema kuwa wasichana hawa pia mara nyingi wanaishi kama wafungwa kwenye nyumba zao huku wakinyimwa ruhusa ya kutoka nje na huenda hata wanapigwa na kunyanyaswa.
Barani Afrika, nchi inayoaminika kuwa na idadi kubwa zaidi ya wasichana wadogo wanaoolewa, mara nyingi kwa lazima, ni Niger ambayo imefikia asilia mia sabini na tano.
Inafuatiwa kwa karibu zaidi na Jamhuri ya Afrika ya Kati na Chad.

Related Posts:

  • LULU ATAJA SEHEMU ZINAZOPATIKANA TIKETI ZA UZINDUZI WA FOOLISH AGE Staa wa filamu za Kibongo Elizabeth Michael‘Lulu’ametangaza rasmi sehemu zinzopatikana tiketi za uzinduzi wa filamu yake ya Foolish Age inayotajiwa kuzinduliwa August 30,Mlimani City,Dar. Lulu ameposti tiketi hizo kupit… Read More
  • KANUMBA FILM, KUSHUSHA KIPYA   Kampuni ya filamu za Kibongo Kanumba The Great Films imeingia mzigoni kuandaa filamu mpya iitwayo WONDER GIRL ikiwashirikisha waigizaji mahiri wa tasnia hiyo.   … Read More
  • FOOLISH AGE YA LULU. TIKETI KUUZWA MLANGONI     Tiketi za uzinduzi wa LULU Bado zinapatikana na Zitauzwa Mlangoni Kwa Gharama za shilingi Elfu 30 tu. UZINDUZI UNAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY KUANZIA SAA MOJA JIONI. usikose wahi sasa … Read More
  • NAY WA MITEGO,MADAM RITA SASA DAMDAM   Mwanamuziki wa Hiphop Bongo,Emanuel Elibarik‘Nay wa Mitego’na Mkurugenzi wa Benchmark Production Rita Paulsen‘Madam Rita hawana tofauti, baada ya kupiga picha ya pamoja katika uzinduzi wa vid… Read More
  • CRAZY GK NA BARAKA AU LAANA Baada ya kupotea kwenye muziki kwa muda mrefu sana Crazy Gk amerudi kwa kishindo na kuzindua wimbo wake mpya huku akisindikizwa na timu ya East Coast Team. Sababu kubwa iliyopelekea King Crazy Gk kupotea kwenye game… Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE