mashabiki waliogawanyika na kuwashindanisha kwa niaba yao,
Team Diamond v/s Team Alikiba,
ushindani ambao umevalishwa ‘mask’ za ‘beef’ ambayo Nasib Abdul
amedai kuwa haipo.
ushindani ambao umevalishwa ‘mask’ za ‘beef’
ambayo Nasib Abdul amedai kuwa haipo.
Platnumz ambaye alikuwa bado hajaamua kuzungumzia tofauti hizo
ameamua kufunguka juu ya ushindani pamoja na ‘beef’
iliyokuwa inazungumzwa baina yake na muimbaji huyo wa ‘Mwana’.
“Nimekua nikiskia muda mrefu vimezungumziwa sana,
kwenye mitandao katika nini,
sijui kwanini vinazungumziwa hivyo” aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm
“Unajua kuna time ikifika inabidi uangalie na kuna vitu uvizoee tu
sababu havikuanza leo hivi vitu sio tu kwa Ali,
ukiwa unafanya vizuri ni msanii yeyote ambaye atakuwepo nae
anafanya nyimbo au akatoa nyimbo
yaani utakuja utashindanishwa nae tu,
Atakuja huyu na huyu na huyu,
lakini wewe mwenyewe tu kuangalia heshima yako iko wapi
kuangalia kazi zako unazifanyaje ubora wake”.
“Tangia mwanzo yaani inavyoanza ishagatokeaga hivyo
ilikua sijui kwa Belle 9, ilitoka kwa Belle 9
ikaja nafikiri sijui Sam Wa Ukweli ilikua,
ikaja sijui kwa Bob Junior,
ikaja pia kwa Ali, ikatoka kwa Ali tena ikaja ikaondoka ikaenda
kwa Omary
I mean Ommy Dimpoz, ikatoka tena ikaja kwa Richard Mavoko,
so kila time inavyokuwa inaenda unafanya vizuri
hivyo vitu vinakua vinatokea,
so ni we mwenyewe kuangalia na watu wasiokuwa na upeo
wanaweza wakahisi hawa watu wana tatizo kumbe si tatizo
ni vitu ambavyo vitakuwepo tu
kwasababu mashabiki wana tabia wakiona mtu
anafanya hichi na we unafanya kitu mkiwa katika kazi
inayofanana hivyo vitu vitatokea yaani watu watashindanisha,
unaweza hata ukashindanishwa
na mtu ambae hata hakufikii kiwango kabisa”.
“Hata kwenye boxing ipo, ukiangalia hata kuna kipindi
ilikuwa TMK na East Coast,
ilikuwaga kwa Dully na T.I.D
hivi ni vitu vya kikazi hata kwenye mpira ndio maana
kuna Simba na Yanga, lakini haimaanishi
Simba na Yanga nimaadui wakikutana Ngassa
ntakupiga ngumi au flani ah ah..”
Diamond amesema kuwa kama Alikiba alikuwa na
tatizo na yeye anaamini angeweza kumfata na
kumwambia sababu amefahamiana nae kabla hajakuwa
mwanamuziki.
“Sasa hivi yaani karibia mwaka wa tano,
Mi tangia nianze kufanya
muziki sijawahi kudrop kila siku nazidi kupanda juu…
so hivyo vitu lazima vitatokea lazima nivikubali,
inawezekana we unasema we unasema we hauna tatizo
lakini mwenzio akawa anahisi wewe una tatizo nae,
lakini naamini kama angekuwa anahisi kama mimi nina
matatizo na yeye angenifata akaniambia kwa sababu
mimi sijajuana na Ali kwenye muziki,
Nimejuana na Ali kabla sijakuwa mwanamuziki,
nimemjua Ali
kupitia dada yangu Queen Darleen so alikuwa ana
uwezo wa
kunifata akaniambia personally kwamba bana
umefanya hichi na hichi na hichi”.
Diamond amemaliza kwa kusema kuwaomba media na
mashabiki wasifanye ionekane kama wana beef binafsi
bali wazishindanishe kazi ili kukuza muziki wa Tanzania.
“Ukiniuliza mimi kiundani kabisa siamini kama kutakua
na tatizola damu ya mtu na mtu,bali ni vitu ambavyo vipo vya kisanaa au vya kimashabiki kwa mashabiki.
Mi nasisitiza sana media na watu wasitengeneze
kufanya kama ni matatizo ya mtu na mtu kwasababu
kisanaa inakua haijengi,
lakini inapokuwa ni baina ya kazi na kazi inakua inasaidia
kwasababu inafanya watu wawe na changamoto
ya kusema
ngoja nitoe kazi kali ili nifanye kitu kizuri inasababisha muziki wetu ukue.”
Chanzo: Bongo5.com
0 MAONI YAKO:
Post a Comment