
Msanii
wa muziki kizazi kipya,Rachael kutoka THT akitumbuiza jukwaani kwenye
usiku wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika katika viwanja lidaz
Club,Kinondoni jijini Dar. Oct 18
Sehemu
ya umati wa watu waliokuwa wakishuhudia yaliyokuwa yakijiri kwenye
jukwaa la Fiesta katika viwanja vya Lidaz Kinondoni
jijini Dar.

Mmoja
wa wasanii wa kike wanaofanya vyema katika anga ya muziki wa
Bongogfleva,Shah akiwa na skwadi lake wakilishambulia jukwaa la fiesta

Mkali
mwingine wa steji,ambae amekuwa akifanya vyema kwenye matamasha
mbalimbali ya fiesta,ukipenda muite Kabyser ama Mr Blue akiimba jukwaani
mbele ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la Fiesta 2014,ndani ya
viwanja vya lidaz club jijini Dar

Mkali
mwingine wa hip hop nchini Mwana-FA akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo
pichani) kwenye tamasha la Fiesta 2014

Kama
kawaida yao wawapo jukwaani,ni kushambulia jukwaa mwanzo mwisho,pichani
kulia ni Stamina na Ney wa Mitego wakikamua jukwaani. Hpa naulizwa Huko kwnu Vip??

Abdulkiba nae akionesha yake jukwaani

Ilikuwa buruuudani kabisa

Pichani msanii Linah (nyeupe) akiwa na skwadi lake mara baada kumaliza kulishambulia jukwaa kwa pamoja.

Anaitwa
Ally kiba ambaye inaelezwa kutoka kwa mashabiki kuwa alifanyo shoo
nzuri na iliyowavutia,na kuthibitisha uwezo wake kuwa ni kweli amerejea
kwenye kiti chake cha usanii.
Mashabiki wakifuatilia tamasha la Fiesta 2014
.

Majina yote mpe yeye,mara Dangote,mara Chibu afu jazia na diamond Platnum akiwa kazini na skwadi lake zima la kazi. Lakini kwa Kiba alikaa

Palikuwa hapatoshi na hayo magamba

Msanii
kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akiwasili kwenye
viwanja vya lidaz club Kinondoni jijini Dar kutumbuiza tamasha la Fiesta
lililofanyika oct 18

Msanii
kutoka nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke a.k.a Davido akiwakuna
mashabiki wake kwa kucheza staili yake ya Skelewi jukwaani,huku miluzi
na shangwe ikiwa imetawala kila kona ya uwanja.


Msanii kutoka nchini Marekani Clifford Haris a.k.a T.I akilishambulia jukwaa la Fiesta vilivyo

NO MEDIOCRE




Mashabiki nao walishangweka kwa raha zao

T.I akiwaimbisha mashabiki wake (hawapo pichani ) na wimbo wake wa NO MEDIOCRE.

Pichani
juu na chini ni sehemu ya umati wa watu wakifuatilia yaliyokuwa
yakijiri kwenye tamasha fiesta lililofanyika katika
viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar.


Ilikuwa ni sheeeddddaaa.

Hapo sasa

Shaha na skwadi lake wakilishambulia jukwaa

Ommy Dimpoz na Victoria Kimani wakilishambulia jukwaa la fiesta 2014

Palikuwa hapatoshi

Victoria Kimani akilishambulia jukwaa

Palikuwa hapatoshi jukwaani kwa kila aina ya burudani

Mmoja
wa askari waliokuwa wamepangwa katika suala zima la kusimamia usalama
ndani ya tamasha la Fiesta 2014 akihakikisha usalama wa kutosha
unakuwepo katika eneo hilo,na watazamaji wanapata burudani iliyokusudiwa
kutoka kwa wasanii mbalimbali waliotumbuiza usiku waTh 18 October

Shaa na madansa wake wakilishambulia jukwaa

Msanii
kutoka THT,Barnaba akiimba wimbo wake wa Wahalade sambamba na madansa
wake kwenye jukwaa la fiesta 2014,katika viwanja vya Lidaz Kinondoni
jijini Dar.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment