January 20, 2015

Maelfu waandamana kupinga kukejeliwa Mtume SAW 

 Maelfu ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Iran leo wameandamana mbele ya Ubalozi wa Ufaransa mjini Tehran kulaani hatua ya gazeti la Charlie Hebdo la Ufaransa ya kuchapishwa tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume wa Uislamu Muhammad (SAW).
Waandamanaji hao walitoa nara dhidi ya gazeti hilo na kutaka kufukungwa balozi wa Ufaransa nchini Iran. Waandamanaji pia wamewataka maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kuchukua hatua dhidi ya kitendo hicho cha kishenzi. 
Maandamano kama hayo ya kulaani kitendo cha kuvunjiwa heshima Mtume Mtukufu yameshuhudiwa pia katika nchi mbalimbalii duniani kama vile Somalia, Pakistan, Niger na Yemen.
 Huko  Chechniya makumi ya maelefu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Grozy kupinga hatua ya gazeti la Charlie Hebdo ya kuchapisha tena vibonzi vinavyomkejeli Mtume SAW. Waandamaji hao walibeba mabango yaliyokuwa yameandikwa ‘Tunayempenda Mtume Wetu.’

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE