Kituo cha kuzalisha na kukuza vipaji(THT) kinatarajia kuadhimisha
miaka kumi tangu kuanzishwa kwake, sherehe hizo zinarajiwa kufanyika
Jan.31, Escape One Mikocheni jijini Dar.
THT ilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2005 kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji, lakini wasio na uwezo wa kujiendeleza wenyewe kwenye sekta ya sanaa hapa nchini, na toka wakati huo kituo hicho kimekuwa na mafanikio makubwa na mchango wa pekee kwenye kukuza sana ya muziki hapa nchini.
Akizungumzia maadhimisho hayo meneja wa kituo hicho, Mwita Mwaikenda alisema ni heshima kubwa kuweza kusheherekea miaka kumi tangu kuanzishwa kwa kituo hicho na kuweza kufanikisha mambo mengi makubwa.
Aidha aliongeza kuwa THT imeendelea kukua kwa kuweza kuanzisha studio yake ambayo imeweza kurekodi matangazo,nyimbo za wasanii wote wa THT pamoja na wengine kama Mdogomdogo na Number One Remix ya Diamond, Me and You ya Ommy Dimpoz, Protoko ya Victoria Kimani na nyingine nyingi.
Aidha katika hatua nyingine THT wameanzisha mafunzo ya ubunifu wa mavazi.
MACHAKU BLOG Inaungana na Taasisi hii katika miaka hii 10 ya mafanikio.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment