Mrembo na
mwigizaji wa filamu, Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ ameamua kufunguka
na kuweka wazi kuwa hayuko tayari kuolewa tena hii ni baada ya kupewa
talaka na aliyekuwa mumewe, Gadna Dibibi.
Jack
alisema, kwa muda aliodumu kwenye ndoa ameshaona raha na karaha yake
hivyo suala la kuolewa tena sasa hivi halipo akilini mwake
“Katika
ndoa lazima kuwe na mabaya na mazuri, hata hivyo siwezi kusema ndoa ni
chungu hapana, ila mimi kwa sasa hivi nimeona nipumzike kwanza sitaki
tena ndoa labda kwa hapo baadaye nitakapojipanga tena upya,” alisema
Jack.Jack
alidumu na mumewe huyo kwa miaka miwili na nusu kabla ya kupewa talaka
hivi karibuni huku chanzo kikiwa ni kusalitiana katika mapenzi.
GPL
0 MAONI YAKO:
Post a Comment