Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNICEF
limetangaza kuwa, vijana wengi wadogo wenye umri wa miaka 13 wametekwa
nyara huko Sudan Kusini.UNICEF imeeleza katika ripoti yake kwamba,
vijana wadogo wasiopungua 89 walitekwa na watu waliokuwa na silaha ambao
walipita majumbani kutafuta watoto wa kiume wa zaidi ya miaka 12.
Baadhi yao walichukuliwa wakati wakiwa wanafanya mitihani. Matukio hayo
yalitokea kwenye kambi katika jimbo la kaskazini la Malakal, ambalo lina
maelfu ya watu waliokimbia vita baina ya wanajeshi wa serikali na
wapiganaji. Pande zote mbili katika vita hivyo wametuhumiwa kuwa
wanatumia watoto vitani. Hivi karibuni Daniel Bekele Mkurugenzi wa
Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch Kanda ya
Afrika alitangaza kuwa, licha ya kuweko ahadi za mara kadhaa za serikali
na wapinzani huko Sudan Kusini za kukomesha utumiaji watoto kama askari
vitani, lakini pande mbili hizo zingali zinaendelea kuwatumia watoto
kama askari.
February 22, 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 MAONI YAKO:
Post a Comment