February 27, 2015

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Tume ya Utumishi wa Umma na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA)
atika uteuzi huo, Rais amemteua Mhe. DKT. STEPHEN JAMES BWANA, Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma na BWANA EDRISSA R. MAVURA, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bw. Mavura ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu.
Sambamba na uteuzi huu, Rais amewateua Makamishna katika Tume hizo, ambapo Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ni
Bwana George D. YAMBESI, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. 
Alhaj Y. F. MBILA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu Bwana Mgeni Mwalimu ALLY, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma iliyomaliza muda wake Bibi Adieu H. NYONDO, Mkurugenzi wa Maadili mstaafu Bibi Salome S. MOLLEL, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu mstaafu, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Bibi Evelyne ITANISA, Katibu Tawala wa Mkoa mstaafu.

Aidha Makamishna wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Bwana Paul Herbert Kinemela, Kamishna wa Kazi, Wizara ya Kazi na Ajira Bwana Mathias Bazi Kabunduguru, Mkurugenzi wa Uendeshaji Sera, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bwana Njaa Ramadhani Kibwana, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (TALGWU) Bwana Jones Kyaruzi Majura, Naibu Katibu Mkuu, Chama Cha Wafanyakazi wa Sekta ya Biashara na Viwanda – (TUICO).
Wengine ni Bwana Jaffari Ally Omari, Mwanasheria Kiwanda cha Sukari – TPC, na Kamishna wa Tume iliyomaliza muda wake Bibi Suzane Charles Ndomba, Afisa Sheria wa ATE na Wakili wa Mahakama Kuu.
Uteuzi huu umeanza tarehe 23 Februari, 2015.

Related Posts:

  • Yanga yaenda Ethiopia bila nyota wake Klabu ya soka ya Yanga imesafiri kuelekea nchini Ethiopia leo Alfajiri ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 na viongozi 13 wakiwemo 8 wa benchi la ufundi. Lakini timu hiyo imesafiri bila ya nyota wake Ibrahim Ajib amba… Read More
  • Uchaguzi TLS, Wakili Fatma Karume amlithi Tundu Lissu   Wakili Msomi Fatma Karume ameshinda nafasi ya Urais wa Chama Cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) na kuwa mrithi wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye amemaliza muda wake leo kutumikia nafasi hiyo kama R… Read More
  • Monalisa aibuka muigizaji bora Afrika   Mona akiwa na mpinzani wake Lupita Nyongo toka Kenya   Mrembo na muigizaji mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama 'Monalisa'  ameibuka mshindi kwenye tuzo za 'The African P… Read More
  • Official video: Bora Nife - Aslay X Bahati Mwanamuziki Aslay kutoka nchini tanzania, amevuka mipaka mpaka kufikia code ya +254 namaanisha nchi jirani ya Kenya na kukutana na mwanamuziki Bahati na kufanya huu wimbo wa Bora Nife.      … Read More
  • Usafiri wa Mwendokasi umesitishwa   Kampuni inayotoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (UDART) imeamua kusitisha usafirishaji wa abiria kwa baadhi ya njia kuanzia saa 11:00 alfajiri kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro eneo la … Read More

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE