Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema yupo tayari kufa kwa kutetea misingi ya haki na utawalawa sheria katika kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu. Alisema hayo jana wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Bustanini, Kiembesamaki, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja katika mkutano ambao waziri wa zamani wa SMZ, Mansour Yussuf Himid aliutumia kutangaza kugombea uwakilishi katika jimbo hilo. Maalim Seif ambaye pi ni Katibu Mkuu wa Chama cha wananchi CUF alisema tayari Jeshi la Polisi limeanza kuweka mizengwe katika upatikanaji wa viwanja vya mikutano ya hadhara kwa madhumuni ya kuibeba CCM, jambo ambalo halikubaliki kwa kuzingatia misingi ya demokrasia. Maalim seif ameongeza kama ninavyomnukuu: “Nakwambieni safari hii kama polisi mmeleta mabomu ya kupiga watu wakati huu wa kuelekea uchaguzi, basi safari hii mtamuua Makamu wa Kwanza wa Rais, sitakubali kuona haki na misingi ya utawala wa sheria ikivunjwa. Mwisho wa kunukuu
Wassira amchongea Mo Dewji kwa serikali kwa kutelekeza mashamba ya Rungwe
-
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen
Wassira ameitaka serikali kupitia Wizara...
The post Wassira amchongea Mo Dewji kwa...
1 hour ago
0 MAONI YAKO:
Post a Comment